Joshua 12

Orodha Ya Wafalme Walioshindwa

1 aHawa ndio wafalme wa nchi ambao Waisraeli waliwashinda na kuitwaa nchi yao upande wa mashariki mwa Yordani, kuanzia Bonde la Arnoni mpaka Mlima Hermoni, pamoja na eneo lote la upande wa mashariki ya Araba:

2 bSihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni.

Alitawala kuanzia Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kuanzia katikati ya bonde, hadi kwenye Mto Yaboki, ambao ni mpaka wa Waamoni. Hii ilijumlisha nusu ya Gileadi.
3 cPia alitawala Araba ya mashariki kuanzia Bahari ya Kinerethi
Yaani Bahari ya Galilaya.
hadi Bahari ya Araba (yaani Bahari ya Chumvi
Yaani Bahari Mfu.
), hadi Beth-Yeshimothi, kisha kuelekea kusini chini ya materemko ya Pisga.

4 fNayo nchi ya Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa mmoja wa mabaki ya Warefai, aliyetawala Ashtarothi na Edrei.

5 gNaye alitawala katika Mlima Hermoni, Saleka, Bashani yote hadi mpaka wa watu wa Geshuri, na watu wa Maaka na nusu ya Gileadi, hadi kwenye mpaka wa Sihoni mfalme wa Heshboni.

6 hMose, mtumishi wa Bwana, na Waisraeli wakawashinda. Naye Mose mtumishi wa Bwana akawapa Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase nchi ya hao wafalme ili iwe milki yao.

7 iHawa ndio wafalme wa nchi ambao Yoshua na Waisraeli waliwashinda upande wa magharibi mwa Yordani, kuanzia Baal-Gadi katika Bonde la Lebanoni hadi kufikia Mlima Halaki, unaoinuka ukielekea Seiri. (Yoshua alitoa nchi zao kwa makabila ya Israeli iwe urithi wao sawasawa na mgawanyiko wa makabila yao:
8
In order to format the table contained in this verse correctly, it has been necessary to move the content of some adjacent verses into it.
,
knchi ya vilima, shefela, upande wa magharibi, Araba, materemko ya milima, jangwa, na Negebu; nchi za Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi):

 9 lmfalme wa Yeriko mmoja
mfalme wa Ai (karibu na Betheli) mmoja
 10 mmfalme wa Yerusalemu mmoja
mfalme wa Hebroni mmoja
 11 nmfalme wa Yarmuthi mmoja
mfalme wa Lakishi mmoja
 12 omfalme wa Egloni mmoja
mfalme wa Gezeri mmoja
 13mfalme wa Debiri mmoja
mfalme wa Gederi mmoja
 14 pmfalme wa Horma mmoja
mfalme wa Aradi mmoja
 15 qmfalme wa Libna mmoja
mfalme wa Adulamu mmoja
 16 rmfalme wa Makeda mmoja
mfalme wa Betheli mmoja
 17 smfalme wa Tapua mmoja
mfalme wa Heferi mmoja
 18 tmfalme wa Afeki mmoja
mfalme wa Lasharoni mmoja
 19 umfalme wa Madoni mmoja
mfalme wa Hazori mmoja
 20 vmfalme wa Shimron-Meroni mmoja
mfalme wa Akishafu mmoja
 21 wmfalme wa Taanaki mmoja
mfalme wa Megido mmoja
 22 xmfalme wa Kedeshi mmoja
mfalme wa Yokneamu katika Karmeli mmoja
 23 ymfalme wa Dori (katika Nafoth-Dori)
Au: katika miinuko ya Nafoth-Dori.
mmoja
mfalme wa Goimu katika Gilgali mmoja
 24 aamfalme wa Tirsa mmoja

wafalme jumla yao ilikuwa thelathini na mmoja.

24
Copyright information for SwhNEN